Mkurugenzi wa Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA), Jamila Mahmoud Juma, akitioa elimu maalum kwa wanafunzi wa shule juu ya masuala ya sheria ya kumliza mtoto
Jumla ya Malalamiko 644, yakiwemo ya utelekezwaji, ulawiti na ubakaji, udhalilishaji kwa watoto katika maeneo mbali mbali visiwani hapa yamepokelewa na Chama cha Wanasheria wanawake Zanzibar (Zafela) kuanzia mwaka 2016 hadi 2019.

Kati ya malalamiko hayo 265 yamepelekwa Mahakamani, 75 yametatuliwa kwa njia za kifamilia, 73 yametatuliwa kwa njia ya ushauri, 115 wahusika wake yamefungishwa mkataba, 41 zimefikishwa Polisi, 27 zimefikishwa ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar,  10 zimefikishwa ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ambapo malalamiko 38 bado hayajapata ufumbuzi .

 Afisa Sheria Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar (Zfela), Khadija Mbarouk Hassan alibainisha hayo huko ofisini kwake wakati akizungumza na mwandishi wa hizi juu ya kazi zilizotekelezwa na Chama chao katika kipindi cha mwaka 2016-2019 kwa maslahi ya jamii na taifa kwa ujumla.

Alisema licha ya ugumu wa kazi yao hiyo lakini wamekuwa wakifanya jithihada mbali mbali za kusaidia jamii katika upokeaji wa malalamiko, kuwapa ushauri, kuwasaidia msada ya kisheria pamoja na shughuli nyengine mbali mbali zenye mnasaba na uanzishwaji wa Chama hicho.

Alitaja mgawanyo wa malalamiko wa liyopokea katika kipindi cha mwaka 2016 ni pamoja na Malalamiko ya Madai ya watoto 90, Malalamiko ya talaka, Utelekezwaji 28, Ulawiti 11, Ubakaji 28, mahari tisa, Kutelekezwa 6, Ujauzito 8, Kipigo 24, Mirath 19, Kukataliwa 7, madai ya mali 30, Huduma 210, madai ya Nyuma 59, Ulaghai moja, madai ya kiwanja 18, kufukuzwa kazi 18 pamoja na madai ya madai ya fedha 21.

Alisema kati ya malalamiko hayo, malalamiko yanahusiana na watoto wamekuwa wakiyapa kipaumbele sana kutokana na kuibuka kwa vitendo mbali mbali vya ubakaji, ulawiti pamoja na utelekezwaji katika maeneo mbali mbali.

Alisema malalamiko hayo wameyapa kipaumbele kutokana na ahari anazozipata mtoto kutokana na matatizo hayo ni kubwa, ambapo baadhi ya wakati hupelekea kwa watoto kufariki duania au kuharibu mifumo yake ya kiakili kutokana na msongo wa mawazo.

Alisema Chama chao kitaendelea kujikita zaidi katika kushughulikia malalamiko ya watoto kwa kutoa kila aina ya ushirikiano wao ikiwa msaada wa kisheria katika vyombo vya sheria pindi ukihitaji ili kuona ustawi wa watoto unazidi kuimarika zaidia.

Alisema katika kufanikisha kazi zao hizo tayari wamepeleka wasiadia wa Sheria katika Wilaya mbali mbali lengo ni kukusanya taarifa za malalamiko na kuzifikisha ofisi kuu ili utaratibu wa kisheria juu ya malalamiko hayo uweze kuchukuliwa.

“lakini pia wasiaidi wetu wa Sheria hupata nafasi ya kutoa elimu kwa jamii juu ya matendo mbali mbali ambayo yakifanyika huwa ni kinyume na sheria za nchi, lengo ni kuona wananchi wanafanya sheria ili waweze kuepukana na matatizo yanaweza kuepukika”alisema.

Khadija aliitaja jamii kuachana kabisa na suala la udhalilishaji, utelekezaji, ubakaji kwa watoto wakijua kuwa sheria namb 6 ya mwaka 2011 ina nguvu kubwa ikiwamo kutoa adhabu ya kifungo kwa mtu atakayetiwa hatiani kwa kosa la udhalilishwaji mtoto.

“Katika kuisaidia jamii juu ya kuachana na matendo ya aina hiyo tumekuwa tukitoa elimu maeneo mbali mbali na tutazidi kutoa elimu hiyo, lengo letu ni kuona ustawi wa mtoto unazidi kuimarika siku hadi siku”alisema.

Baadhi ya wananchi ambao wamekumbwa na mtatizo mbali mbali yakifamilia na kindoa, walisema licha ya kupatwa na matatizo hayo lakini wanashindwa kutoa taarifa sehemu husika kutokana na ukosefu wa elimu pamoja na kutozitambua ofisi za wasaidizi wa Sheria.

Mmoja wa wananchi hao ni Bi Safia Nassor Mbarouq (61) mkaazi wa Masingini Wilaya ya Magharib ‘A’ Unguja ambaye ametelekezwa akiwa na watoto wanane, amesema ameshindwa kufika katika vyombo kama hivyo ili kupata msaada wa kisheria kutokana na kufahamu vyema uwepo wake pamoja na maeneo husika zilipo ofisi zake.

Imeandikwa na Haji M. Mohd, chini ya ufadhili wa UNICEF

Facebook Blogger Plugin by Piere
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post a Comment

 
Top