Katibu
Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amepewa onyo kali
pindi akishiriki katika kampeni za uchaguzi za kumnadi mgombea ubunge wa Jimbo
la Kinondoni kupitia Chama cha Chadema na kuacha kumnadi mgombea waliyeteuliwa
na Chama chake cha CUF katika Jimbo hilo.
Mkwala
huo umetolewa na Kamanda Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF upande unamuunga mkono Profesa
Ibahim Lipumba Thiney Juma ambaye aliibuka na kutoa kauli hiyo baada ya kuwepo kwa
taarifa kuwa huenda Maalim Seif akaibuka katika mikutano ya Chadema na kumnadi
mgombea wa Chadema.
Thiney
alisema kuwa pamoja na kuwepo kwa taarifa kuwa Maalim Seif huenda akamnadi
mgombea huyo lakini atambue kuwa kufanya hivyo ni makosa makubwa kwa mujibu wa
katiba ya CUF.
“Yeye
ni kiongozi wetu mkubwa tu na anafahamu vizuri sana katiba ila tunasikia kama
huenda akamnadi mgombea wa Chadema ila akisubutu kufanya hivyo kamati ya
nidhamu lazima ichukue mkondo wake dhidi yake hasa kwa kuwa atakuwa amekiuka
katiba yetu”alisema Thiney.
Thieney
alisema kuwa kama Maalim Seif ana hamu ya kupanda jukwaani anaruhusiwa kupanda
jukwaa la CUF katika Jimbo hilo hilo la kinondoni ambapo pia CUF nao wana
mgombea wao katika kinyang’anyiro cha Ubunge.
Alisema
kuwa hadi sasa wao kupitia vikao mbali mbali hawajachukua hatua yoyote ya
kumtaka kiongozi huyo asishiriki kwenye kampeni za Chadema akisema kuwa Maalim
Seif anajua wajibu wake kama kiongozi wa muda mrefu kwenye chama hicho.
“Maalim
tunamtambua sana kama kiongozi wetu na ilipanswa yeye ndiye atongoze sisi sio
sisi tumuongeze yeye katika hili la kukiuka katiba ya Chama chetu’alisema.
Aliongeza kusema kuwa “Sisi tunashangazwa sana
kuona kiongozi wetu huyo pamoja na kuwa na umri mrefu katika Chama lakini
amekuwa ni mtu wa kushangaza kwa kufanya mambo yanayokwenda kinyume na katiba
za Chama “alisema.
Alisema kuwa milango ipo wazi kwa Maalim
kuachana kabisa na dhana yake hiyo akitambua kukaa pindi akithubutu kwenda
kinyume na katiba ya Chama hatua za kisheria dhidi yake zitafuata bila ya
kuoneana muhali.
Facebook Blogger Plugin by Piere
Post a Comment