Katika kuhakikisha vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia hasa kwa wanafunzi vinamaliza, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali imesema imejipanga katika kutoa elimu ya udhalilishaji na ukatili kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari Unguja na Pemba.
Mkurugenzi Elimu na Maandalizi kutoka
Wizara ya Elmu Zanzibar, Safia Ali Rijali alibainisha hayo visiwani hapa ikiwamo ni moja ya jitihada za kukabiliana
na matendo hayo ambayo yamekuwa ni tishio kubwa hasa kwa watoto wakiwamo
wanafunzi.
Alisema mpango huo wa kutoa elimu
mashuleni umekuja baada ya kuonekana vitendo hivyo kukithiri , huku kundi
la wanafunzi nalo lilikubwa na vitendo hivyo ambavyo baadhi ya wakati hurudisha
nyuma jitihada za elimu kwa wanafunzi wanaokumbwa na kadhia hiyo.
Alisema lengo kuu la elimu kwa anafunzi
ni kuwawezeha kufahamu kwa kina suala au viashia vya udhallishaji na ukatili
pamoja na madhara yake, ili kila mwanafunzi kuwa na elimu ya kujikinga navyo
pindi akionesha ishara ya vitendo hivyo.
Alisema mbali ya elimu hiyo ya kina kwa
wanafunzi mbali mbali lakini pia Wizara imepanga kuanzisha vikundi maalumu vya
kutoa elimu ya udhalilishaji ambavyo vitatumika katika kusambaza elimu na
kusimamia udhalilishaji ndani ya Shule.
“Lakini pia tumepanga kuzipa elimu hiyo kamati
za Shule zinazosimamia Elimu pamoja na kutoa Elimu kwa walimu katika Shule hizo
juu ya namna ya kusimamia matendo hayo ili yasitokee katika shule zetu”alisema.
Hata hivyo alisema katika kipindi cha
mwezi miezi sita Januari hadi Juni mwaka jana Wizara ya Elimu
ilipokea kesi 30 za udhalilishaji kwa watoto
ambapo kesi 10 ambapo Unguja zilikuwa 4 na Pemba 6.
Alisema kwa upande wa kesi za ubakaji
zilikuwa 5 ambapo Unguja ilikuwa kesi 1 na Pemba kesi 4 pamoja na kesi za
11 za Ujauzito kwa wanafunzi hao ambapo Unguja 8 na Pemba 3.
Kwa upande wa Sheikh Ali Abdallah Amour
kutoka Jumuiya ya Maimamu Zanzibar alisema kushamiri kwa vitendo hivyo vya udhalilishaji
na ukatili kwa watoto vinatokana na jamii kuacha utamaduni wao na kufuata
tamaduni za kigeni.
Alisema umefika wakati sasa kwa wazazi na
walezi kuunga kwa pamoja katika kulea watoto kwa kufuata malezi yalio bora hasa
kwa kufuata misingi ya dini ili kuwa jamii iliyo bora, huku akibainisha kuwa
pindi kila mmoja akifuata njia hiyo ni wazi kwamba vitendo hivyo vinaweza
kuondoka.
Kwa Upande wake Mwanaharakati wa kupambana
na vitendo vya ukatili na udhalilishaji kwa wanawake na watoto Nassor
Hamadi alisema kuwa ili vitendo vya ukatili na udhaliliishaji kwa watoto
vikomeshwe Zanzibar Serikali haina budi kusimamia Sheria zake.
Alisema nchi ina sheria nzuri sana ambazo
zinamlinda mtoto kikubwa kinachokosekana ni kuzisimamia Sheria hizo kwa wale
wafanyaji wa matendo hayo ni kuchukulia hatua za haraka.
Imeandikwa na Haji M. Mohd, chini ya ufadhiliwa UNICEF
Facebook Blogger Plugin by Piere
Post a Comment