Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Ofisi ya Mtakwim Mkuu wa Serikali Zanzibar wanatarajia kuanza utaratibu wa kutangaza takwim za matukio ya ajali mbali mbali yanayowapata watoto visiwani Zanzibar.

Utaratibu huo unatarajiwa kuanza wakati wowote kuanzia sasa baada ya taratibu za pande mbili hizo kukamilika, ambapo kwa kila mwezi watakuwa wakitoa takwim hizo.

Khamis Juma Khamis kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Zanzibar kikosi cha Usalama babarani aitoa kauli hiyo huko Mazizini Mjini Unguj, ambapo alisema tayari wameshafanya mazungumzo kati yao ofisi ya Mtakwim pamoja an wadau wa masuala ya watoto na kuona kuwa kuna kila sababu ya takwim za matukio ya ajali kwa watoto kutangazwa.

Alisema licha ya hivi sasa Jeshi la Polisi kushirikiana na ofisi ya Mtakwim kutoa takwim za matukio ya ajali kwa kila mwezi kwa kuangalia kundi la watu wazima tu, lakini wameona ni vyema kundi la watoto nalo likawekwa ndani ya mpango huo.

Alisema lengo ni kuwawezesha wananchi kujua idadi ya matukio yaliowakumba watoto katika kipindi cha mwezi mzima, ili kwa wale wadau wanaoshughulikia masuala ya utetezi wa watoto itakuwa ni msaada kwao katika majukumu ya kazi zao hizo.

Hat hivyo alisema jitihada mbali mbali zinafanyika katika kuhakikisha suala la usalama barabarani linaendelea kudhitiwa, ikiwamo kufanya doria , lengo ni kuona idadi ya matukio ya ajali na makosa ya barabarani yanapungua.

Alitumia fursa hiyo kuwaomba madereva wa vyombo vya moto kuendelea kufuata sheria za usalama barabarani ili kuona idadi ya ajali zinapungua, huku akibainisha kuwa hawatakuwa tayari kuona kuna dereva anavunja sheria.

Naye Mtakwim kitengo cha cha Takwimu za makosa ya Jinai, madai na jinsia kutoka Afisi kuu ya Mtakwim Mkuu wa Serikali Zanzibar, Asha Mussa Mahfoudh alijusema jumla ya ajali 25 zimeripotiwa katika kipindi cha mwezi wa Disember 2019 ikiwamo ni pungufu ukilinganisha na ajali 33 kwa mwezi wa November.

Alisema katika ajali hizo jumla ya waathirika  42 wameripotiwa wakiwemo wanawake 10 sawa na asilimia 23.8 na wanaume 32 sawa na asilimia 76.2, ambapo waliofariki ni 14, wanaume 9 na wanawake watano.

“Lakini pia kulikuwa na majeruhi 28, wanaume alikuwa ni 23 na wanawake walikuwa ni watano, hivyo bado tunasisitiza madereva kuwa waangalifu sana wanapotumia vyombo vya moto”alisema.

Hata hivyo alisema kwa kipindi cha mwaka mzima ajali zilizotokana na makosa mbali mbali zilikuwa ni 301 ikiwa zimepungua kwa asilimia 6.5 ukilinganisha na ajali 322 mwaka 2018.

“Idadi ya waathirika mwaka 2019 imepungua kwa asilimia 13.8 kutoka waathirika 645 mwaka 2018, huku Wilaya ya Mjini Unguja Magharib ‘A’ na ‘B’ pamoja Wete zikiripitiwa ajali nyingi ukilinganisha na Wilaya nyengine”alisema.

Imeandikwa na Haji M. Mohd

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top