MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) kanda ya Zanzibar, imefanikiwa kukushanya shilling billion 61.6 sawa na asilimia 92 ya makadirio ya mapato katika kipindi cha Oktoba 2017 hadi Disemba 2018.
Naibu Kamishna wa Mamlama hiyo, Mcha Hassan Mcha, aliyasema hayo wakati akizungumza na mwandishi wa gazeti hili ofsini kwake Gulioni.
Alisema makadirio ya awali katika kipindi hicho yalikuwa ni kukushanya shilingi bilioni 66.8 kiwango ambacho hakikufikiwa.
Aidha alisema kushuka kwa kiwango cha ukushanyaji mapato kunatokana na kupungua uingizaji bidhaa kutoka nje.
Alisema kwa upande kodi zinazotokana na bidhaa ziliomo ndani kama vile maduka, alisema wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Hata hivyo, alisema katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Januari 2018 hadi Machi, Mamlaka hiyo inatarajia kukushanya shilling bilioni 66.8 ambapo mwezi wa Januari wamekusanya shilingi bilioni 21.4, Februari wanatarajia kukushanya shilingi bilioni 21.3 na Machi shilingi bilioni 21.7.
Alisema katika kuhakikisha fedha hizo zinakusanywa wanaendelea kutoa elimu kwa wafanyabishara pamoja na taasisi mbali mbali kuhusu umuhimu wa kulipa kodi na kuzuia kodi ya serikali.
chanzo, Zanzibar leo
Facebook Blogger Plugin by Piere
Post a Comment