PAZIA la Mashindano ya Kombe la Mapinduzi linafunguliwa leo Ijumaa Disemba 29, 2017 katika uwanja wa Amaan.

Katika ufunguzi huo kutafanyika michezo mitatu ambapo saa 8:00 za mchana wataanza  Mlandege dhidi ya JKU, Saa 10:00 za jioni Jamhuri watacheza na ndugu zao Mwenge na  saa 2:15 usiku Zimamoto watakipiga na Taifa Jang’ombe.

Jumla ya timu 11 zitakazoshiriki Mashindano hayo zikiwemo sita za Zanzibar, nne kutoka Tanzania bara na moja kutoka Uganda ambapo zimepangwa katika makundi mawili A na B.

Katika michuano hiyo klabu ya Yanga ambayo ipo katika kundi B, ipo pamoja na timu za Zimamoto, Mlandege, JKU, Taifa  Jang’ombe na Singida United .

Wakati  kundi A, lina timu za mabingwa watetezi Azam FC, Simba SC, URA, Mwenge na Jamhuri.
Mbali na michezo hiyo ya leo rataiba hiyo itaeandelea tena Disemba   30, 2017 Jumamosi saa 10:00 Zimamoto  na  JKU, Saa 2:15 usiku  Taifa  Jan’gombe itacheza na  Mlandege.

Disemba  31,2017 Jumapili Saa 10:00 Azam itacheza na  Mwenge  na  saa 2:15 usiku Jamhuri itakwaruzana na  URA, wakati Januari  1, 2018 Jumatatu Saa 10:00 Mlandege na   Zimamoto  na  saa 2:15 JKU  Taifa ya Jan’g

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top