WANAFUNZI 122 kutoka nchi mbali mbali duniani wamejiunga na Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kwa mwaka 2016/2017. 

Kati ya wanafunzi hao 59 waliingia mwaka 2016 na 63 mwaka huu wakitokea vyuo mbali mbali duniani kama  Boston cha Marekani, Hamburg cha Ujerumani, Haukeland cha Norway na  SOAS cha Londan, Uingereza.

Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili, Kaimu Mkuu wa Idara ya Kiswahili na Lugha za Kigeni, Shani Suleiman Khalfan, alisema hata hivyo, idadi ya wanafunzi imepungua kwa sababu bado Zanzibar haijakitangaza Kiswahili ipasavyo nje ya nchi.

Aidha alisema machafuko ya Libya yamechangia idadi ya wanafunzi kupungua kwa sababu nchi hiyo ndio ilikuwa inaleta wanafunzi wengi na walikuwa wanakaa muda mrefu.

Alisema tatizo jengine ni kuwepo walimu wengi binafsi wanaofundisha Kiswahili ambapo wageni hao badala ya kujiunga na taasisi hiyo kuamua kuwatafuta walimu hao ili kuwasomesha.

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top