Mabingwa wa ligi kuu Zanzibar timu ya JKU wameanza vibaya mashindano ya kombe la Mapinduzi baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa vijana wa timu ya Mlandege.

Mchezo huo ulikuwa ni waufunguzi rasm wa michuano hiyo ulipigwa katika uwanja wa Amaan mjini Unguja leo na kushuhudiwa na mamia ya washabiki na wapenzi wa soka visiwani humu.

Wakati JkU ikilala kwa bao hizo mchezo wa pili unaendelea kati ya timu ya Jamhuri na Mwenge ambapo wakati wa usiku leo Zimamoto watavurumishana na timu ya Taifa ya Jang’ombe.

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top