Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ZEC
imeandaa rasimu ya mtaala wa elimu ya wapiga kura ambao utatumika kwa
taasisi zinazotakutoa elimu ya wapiga kura baada ya kupewa kibali na
tume cha kutoa elimu.
Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Mhe. JOKHA
KHAMIS MAKAME alieeleza hayo katika ukumbi wa mikutano wa Tume hiyo
wakati akifungua mkutano wa kujadili rasimu ya mtaala wa Elimu ya Wapiga
Kura.
Alisema matayarisho ya Mtaala huo
yanatokana na maelekezo ya kifungu cha 106(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya
Zanzibar Nam. 4 ya mwaka 2018 yanayoitaka Tume kutayarisha mtaala wa
Elimu ya Wapiga Kura utakaotumiwa na Wadau wa Uchaguzi wanaotaka kutoa
Elimu ya Wapiga Kura.
Mshauri elekezi JUMA HAJI USSI alisema
Tume kwa upande wake inatarajia utekelezaji wa mtaala huo wa elimu
utawasaidia wadau wa uchaguzi wakiwemo washirika wa maendeleo,
Waangalizi wa Uchaguzi, Vyama vya Siasa na Asasi za Kiraia ambapo lengo
la mtaala huo ni kuwajengea uelewa na kuangalia kwa kiasi gani elimu
hiyo itawafikia walengwa.
Ndugu Juma alisema Mtaala huo
umeainisha misingi ya utoaji wa elimu ya Wapiga kura pamoja na Sheria ya
uchaguzi ya Zanzibar ambayo imetoa mamlaka ya kuratibu, kusimamia, na
kuendesha elimu ya Wapiga Kura kwa mujibu wa Sheria ya uchaguzi ya
Zanzibar ya Nam. 4 ya mwaka 2018.
Alifahamisha kuwa utayarishaji wa mtaala
huo, pia ulifanyika kwa kuzingatia vigezo vya kisheria na
ushirikishwaji wa makundi ya kijamii ili umsaidie Mzanzibari kupata
elimu bora inayohusu Demokrasia katika masuala ya kiuchaguzi.
Washiriki wa mkutano huo wameipongeza
Tume kwa kuandaa mtaala ambao umekidhi vigezo na kuzingatia umuhimu wa
makundi mbalimbali katika masuala ya Uchaguzi
Rasimu ya mtaala wa elimu ya Wapiga Kura
umeainisha makundi mbali mbali ambayo yanahusika moja kwa moja katika
ushiriki na ushirikishwaji wa masuala ya uchaguzi wakiwemo Vyama vya
Siasa, Asasi za Kiraia, Makundi Maalum na vyombo vya habari
Facebook Blogger Plugin by Piere
Post a Comment