Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Zoezi la uandikishaji na uhakiki wa taarifa za Wapiga kura limeanza rasmin katika Wilaya ya Magharib “A” pamoja na Jimbo la Kiwengwa, Mahonda na Bumbwini kwa Wilaya ya Kaskazini “B”
Wakizungumza katika vituo vya
Uandikishaji baadhi ya Masheha wakiwa ni Mawakala wa Tume wamesema
maandalizi mazuri ya Tume na kuimarishwa ulinzi na usalama katika vituo
vyote kumesababisha wananchi kuhamasika na kujitokeza kwa wingi katika
zoezi hilo.
Walisema pia, Utoaji wa Elimu na
upatikanaji wa taarifa kwa wananchi kupitia vyombo vya habari na
viongozi wa Shehia nako kumesaidia kutoa hamasa kwa wananchi kushiriki
kujiandikisha na kuhakiki taarifa zao.
Zoezi la Undikishaji na Uhakiki wa
taarifa za Wapiga Kura kwa Wilaya ya Magharibi “A” pamoja na majimbo
matatu ya Wilaya ya Kaskazini “B” litamalizika jumatatu ya tarehe
24/2/2020.
Wakati huo huo Wadau wa uchaguzi
walishauri kuwa Matukio ya kiuchaguzi yanahitaji uvumilivu na
ushirikiano baina ya Wadau wa Uchaguzi ikiwa pamoja na kutoa elimu ya
wapiga kura ili kudhibiti na kutatua changamoto ambazo hujitokeza wakati
wa Uchaguzi.
Ushauri huo ulitolewa na wadau hao
katika Mkutano ulioandaliwa na Tume ya uchaguzi ya Zanzibar ukumbi wa
kituo cha walimu Kiembe Samaki ukiwa na lengo la kutoa elimu kwa wadau
wa Uchaguzi juu ya umuhimu wa zoezi la uandikishaji na uhakiki wa
taarifa za Wapiga Kura.
Aidha, waliendelea kusema kuwa
ushirikishwaji wa Wadau wa Uchaguzi katika hatua mbalimbali za uchaguzi
utasaidia kupunguza changamoto na malalamiko ya wananchi ambayo
hujitokeza kabla, wakati na baada ya Uchaguzi.
Akitoa ufafanuzi wa hoja
zilizowasilishwa na wadau wa Uchaguzi katika mkutano huo Afisa
Uandikishaji Wilaya ya Kusini MBARAKA SAID HASOUNI alisema, Tume
itaendelea kufanya kazi zake kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na miongozo
iliyopo na kuhakikisha inazitafutia ufumbuzi changamoto zinazojitokeza
wakati wa uchaguzi.
Afisa Uandikishaji Wilaya ya Mjini SAFIA
IDDI MOHAMMEDI alisema huduma za uendelezaji wa Daftari la Kudumu la
Wapiga Kura ambazo ni kuhamisha taarifa, kurekebisha taarifa na
kushuhulikia maombi ya waliopoteza Vitambulisho vya Kupigia kura
hazitofanyika katika katika vituo vya Uandikishaji badala yake huduma
hizo zitafanyika katika Ofisi za Uchaguzi za Wilaya mara baada ya
kumalizika kazi ya Uandikishaji na Uhakiki wa taarifa za Wapiga Kura
Vituoni.
Mkutano wadau wa Uchaguzi Wilaya ya
Magharib "B" ni Mkutano wa kumi katika muendelezo ya mikutano ya wadau
wa uchaguzi wa Wilaya iliyoandaliwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar
ikiwa ni maandalizi ya Uandikishaji na Uhakiki wa taarifa za Wapiga Kura
kwa mpangilio wa Wilaya.
Facebook Blogger Plugin by Piere
Post a Comment