RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amesema kuwa kuwepo kwa mazingira ya muhali katika jamii kumeweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kudhorotesha mienendo ya kesi za udhalilishaji wa wanawake na watoto.

Hayo aliyasema leo, Ikulu Jijini Zanzibar alipokutana na uongozi wa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wanawake na Watoto wakati ilipowasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mpango Kazi kwa kipindi cha Julai hadi Disemba katika mwaka wa fedha 2019/2020.

Rais Dk. Shein alieleza haja ya kuachana na muhali katika kuzitafutia ufumbuzi kesi za udhalilishaji wa wanawake na watoto na kusisitiza umuhimu wa kusimamia sheria na kutaka sheria kuchukua mkondo wake ili kuondoa malakamiko katika jamii.

Alieleza kuwa juhudi za makusudi zimechukuliwa na Serikali ikiwa ni pamoja na kuunda Kamati Maalum ya kupambana na vitendo vya ushalilishaji wa wanawake na watoto hivyo kuna kila sababu ya kuchukuliwa hatua za kisheria kwa wanaofanya vitendo vya udhalilishaji huo.

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top