Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jaji Mkuu Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid amewataka wale wote waliokuwa hawana vitambulisho vipya vya mzanzibar mkaazi,kufanya hima ya kuvifatilia vitambulisho hivyo ili kuwa na sifa ya kuandikishwa pamoja na kufanyiwa uhakiki katika daftari la kudumu la wapiga kura.
Jaji Hamid alitoa kauli hiyo katika ziaza
yake ya kutembelea vituo vya zoezi la uandikishaji pamoja uhakiki katika
daftari la kudumu la wapiga kura huko Wilaya ndogo ya Tumbatu Mkoa Kusini
Unguja.
Alisema ni jambo na busara kwa wale ambao
hawana vitambulisho vipya vya mzanzibar vilivyofanyiwa uhakiki, kufanya uharaka
wa kwenda kuvitafuta vipya ili kutumia fursa yao ya kisheria ya kuandikishwa
pamoja na kufanyiwa uhakiki katika daftari la wapiga kura.
Alisema tume inaendelea na kazi yake ya
kufanya ya uandikishaji wa wapiga kura wapya na uhakiki wa taarifa za wapiga
katika Wilaya mbali mbali kwa kuwahusisha wale tu waliopata vitambulisho vipya
vya mzinzibar mkaazi, huku akisisitiza kuwa kwa wale ambao hawana vitambulisho
vipya bado wana fursa ya kuandikishwa pindi kiwavipata vitambulisho hivyo.
Hata hivyo alisema Tume ya Uchaguzi ya
Zanzibar (ZEC) baada ya kukamilika kwa zoezi hilo itafanya tathmini ili
kuangalia kwa namna ambavyo itaweza kusaidia kuzitatua changamoto za Wananchi
ambao watakosa fursa ya kuandikishwa katika Daftari kutokana na sababu ya
kukosa Vitambulisho vya Mzanzibar Mkaazi.
Alisema lengo la ziara hiyo ni kupata
tathmini ya awali ili kujua mafanikio na changamoto juu ya utaratibu wa
uandikishaji na uhakiki wa taarifa za wapiga kura unavyoendelea.
Naye Afisa uandikishaji Wilaya ya
Kaskazini ‘B’, Makame Pandu Khamis alisema zoezi la Uandikishaji wa Wapiga Kura
Wapya na uhakiki wa taarifa za Wapiga Kura linaendelea vizuri katika vituo vyote
vya Wilaya ya Kaskazini “A”.
Alisema zoezi hilo linaendelea vizuri
kutokana na maandalizi na juhudi zinzochukuliwa na Watendaji wa Tume pamoja na
Masheha wa Shehia kuhamasisha Wananchi wao kwenda katika vituo kujiandikisha na
kuhakiki taarifa zao.
Aliongeza kusema kuwa, mpaka sasa Vituo
vyote 33 vya Wilaya ya Kaskazini “A” pamoja na Vituo tisa vya Jimbo la Donge
kuna Idadi Kubwa ya Wananchi waliojitokeza kuandikishwa na kuhakiki taarifa zao
mbali na baadhi ya changamoto ndogo ndogo zilizojitokeza vituoni ambazo
zilirekebishwa kwa kupewa maelekezzo wapiga kura kwenda katika vituo ambavyo
zipo taarifa zao.
Alieleza kuwa amani na utulivu umetawala
katika Vituo hivyo ambapo aliwataka wananchi hususan Vijana ambao wametimiza
sifa za kuwemo kwenye daftari kwenda kujiandikisha na kwa wale waliokuwemo
katika Daftari kwenda kuhakiki taarifa zao kwani bila kufanya hivyo hawatoweza
kupiga kura kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
Katika hatua nyengine Mkurugenzi wa
Uchaguzi, Thabit Idarous Faina amewataka wananchi kuutumia vizuri muda kutokana
na mfumo unaotumika kuandikisha wananchi na kuhakiki taarifa za Wapiga Kura
unatumia muda mdogo sana wastan wa dakika moja mpaka mbili kwa mwananchi mmoja.
Alisema Tume ya Uchaguzi itamuandikisha
kila mwananchi aliyetimiza sifa za kuandikishwa katika Daftari la Kudumu la
Wapiga Kura kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar Nam. 4 ya mwaka 2018
ili kuweza kupiga kura katika Uchaaguzi Mkuu wa 2020.
Kwa upande wa baadhi ya wananchi
waliiomba Tume ya Uchaguzi kaungalia uwezekano njia nyengine mbadala ya
kuandikishwa katika daftari hilo badala ya kutumia kitambulisho kipya cha
mzanzibar.
Facebook Blogger Plugin by Piere
Post a Comment