MAHAKAMA ya wilaya Wete imemhukumu kwenda chuo cha mafunzo kwa kipindi cha miaka saba, Mgeni Amour Kombo, (Bihaloo) mwenye umri wa miaka  32 na mwezake Hafidh Khamis Amour mwenye umri wa 36 wote wakaazi wa Mkoa wa Kusini Pemba, baada ya kupatikana na hatia ya kosa la dawa za kulevya.

Mahakama hiyo chini ya hakimu Abdalla Yahya  Shamhuna na Mwendesha mashtaka Juma Ali Juma iliwatia hatiani  na kuwataka kutumikia chuo cha mafunzo kwa muda huo baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.

Washtakiwa walipatikana na kete 48 za dawa za kulevya aina ya heroin zenye uzito wa gramu 0.42.
Mahakama hiyo pia  imewataka kulipa faini ya shilingi milioni tano kila mmoja.

Aidha mbali na  adhabu hiyo , pia mahakama imeamuru kuitafisha gari waliyoitumia kusafirisha dawa hizo.

Mapema mwendesha mashtaka, Juma Ali Juma, aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa washtakiwa ili iwe fundisho kwao  na wengine wenye tabia kama hiyo.
Chanzo Zanzibarleo

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top