JUMLA ya wastaafu 6,764 wamefanyiwa uhakiki kupitia Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF), kuanzia Januari Mosi hadi 29 mwaka huu kati ya wastaafu 8,000.
Hayo yalielezwa na Ofisa wa Mafao wa ZSSF, Zainab Rajab Baraka, lipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi huko Ofisini kwake Kilimani mjini Unguja jana.
Alisema wanachokizingatia kwa wastaafu kwamba wanatakiwa kufanya uhakikini kuthibitisha kwamba mstaafu yuko hai, na pensheni inapopelekwa na ZSSF inamfika mlengwa anayehusika.
Alisema hiyo inaisaidia ZSSF kutotoa fedha kwa wastaafu hewa kwa sababu imegundulikana wapo wastaafu ambao wameshafariki na inawezekana kwa namna moja ama nyengine familia haijui kama inatakiwa ikatoe taarifa katika mfuko ikiwa mstaafu ameshafariki ili pensheni yake ipate kuzuliwa.
Ofisa huyo, alisema, wengi wao wanachukuwa nafasi hiyo kuona fedha inaingia na pengine mtoto ana fursa ya kutoa benki na kwenda kuchukua fedha na kuendelea na mambo yake.
Alisema kuwepo kwa uhakiki kila baada ya miezi sita kutawasaidia kujua nani yupo na nani hayupo, pia asipokwenda ZSSF itajua huyo mtu hayupo tena na kikubwa itawasidia kuzuia mafao kupotea.
“Asipo kwenda kuhakikiwa itakuwa aidha amefariki au yuko nje ya nchi, na ambae amesafiri anatakiwa kwenda kuhakiki fedha zao zinaendelea kuingia benki.
Alisema changamoto ambayo iliyopo kwa kipindi hiki kwa sababu ZSSF ilifanya mabadiliko ya utoaji wa pensheni kwawastaafu waliokuwa wakipokea pensheni dirishani kuanzia mwezi wa Novemba wametakiwa kufungua akaunti katika benki ili ZSSF ipate kupunguza mzigo wa kukaa na pesa nyingi ofsini kwa lengo la kutafuta ulinzi ili kujikinga.
Alisema unapofungua akaunti benki unatakiwa ujijue kuwa wewe ni mtaafu ambao unatakiwa kuhakiki kila inapofika Januari na Julai, lakini wengi wa wastaafu ambao waliokuwa wanapokea dirishani ama hawakuzingatia, au hawakuskia kuhusiana na uhakiki.
chanzo Zanzibae leo
Facebook Blogger Plugin by Piere
Post a Comment