Wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa nchini
Zanzibar kutoka nchi mbalimbali wametakiwa kufuata sheria na
taratibu zilizowekwa za uingizaji wa biashara ikiwemo kuzisajili
bishaa na kufanyiwa uchunguzi kabla hawajazisambaza sokoni ili
kumlinda mtumiaji kutopata madhara.
Akizungumza na wakala wa forodha na
wafanyabiashara wa chakula,dawa,vipodozi na vifaa tiba Mkurugenzi
Mtendaji wa Wakala wa chakula,dawa,vipodozi na vifaa tiba Zanzibar
katika ukumbi wa mkutano Kidongo chekundu mjini Unguja Burhani Othman
Simai amesema kupitia sheria namba 3 ya chakula,dawa na
vipodozi itaweza kusaidia katika kudhibiti wafanyabiashara kuingiza
bidhaa nchi zisizo na ubora na viwango kwa watumiaji.
Amesema imebainika kuwepo kwa
wafanyabiashara kukiuka taratibu zilizowekwa na serikali nchini ya
taasisi hiyo ya wakala wa chakula dawa na vipodozi kwa kuingiza bidhaa
zisizostahiki na kupelekea athari mbalimbali wa wananchi wa Zanzibar
ambao ni watumiaji wakubwa.
Hata hivyo Burhani amesema
Wakala hatokubali kuona nchi inaingizwa bidhaa
zilizombovu lazima zifanyiwe ukaguzi na kusajiliwa kabla ya
kutumiwa ili bidhaa zote zinazoingizwa ziwe na ubora kuanzia
viwandani.
Kwaupande wao baadhi ya Wafanyabiashara hao
wakizungumza na Zanzibar24 wameziomba taasisi zinazohusika na udhibiti
wa ubora wa bidhaa ikiwemo ZBS,Mkemia mkuu na Wizara ya Afya kuandaa
sheria watakayoitumia pamoja ili kuondoa migongano ya kisheria wao
na wafanyabiashara wanaoingiaza bidhaa nchini.
Wamesema nivyema sasa serikali
kujipanga kuzifanyia maboresho maabara zao za ukaguzi wa bidhaa kuweza
kufanya kazi kwani imeonekana kutokuwa na uwezo katika utendaji ndio
maana wafanyabiashara wengi hukwepa kupeleka bidhaa zao na kutafuta
maabara ambazo wataona zina mapato Sokoni.
Mkutano huo wenye lengo la
kuwatambulisha wafanyabiashara mabadiliko ya mfumo wa kiuchumi kutaka
bidhaa zote zipate ithibati za kimataifa ili kuingia katika masoko
makubwa ya kimataifa.
chanzo, Zanzibar 24
Facebook Blogger Plugin by Piere
Post a Comment