DEREVA wa gari ya abiria iliyopata ajali katika kijiji cha Kikungwi wiki mbili zilizopita, Haji Wakili Haji (45) mkaazi wa Makunduchi, amefariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Mnazimmoja.

Dereva huyo ni miongoni mwa majeruhi waliopata ajali iliyotokea Januari 15 mwaka huu katika kijiji hicho baada ya kugongana na gari nyengine ya abiria.

Msaidizi wa kitengo cha huduma kwa wateja katika hospitali hiyo, Mwanaisha Mhammed Khamis, alisema hayo wakati akizungumza na Zanzibar Leo.

Alisema majeruhi huyo alikuwa hospitalini hapo akiendelea na matibabu lakini hali yake ilikuwa si nzuri kutokana na kuumia sehemu mbali mbali za mwili wake.

Aidha alisema majeruhi wengine bado wapo hospitalini hapo wakiendelea kupatiwa matibabu.
Kufa kwake kunafanya idadi ya watu waliokufa kufuatia ajali hiyo kufikia watatu.
chanzo Zanzibar leo

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top