KATIKA kujenga na kudumisha udugu ulipo baina ya Serikali ya Watu wa China na Zanzibar, Madaktari bingwa wanaofanya kazi zao katika Hospitali ya Abdalla Mzee Pemba, wamekabidhi vifaa vya mchezo wa mpira wa Kikapu kwa klabu ya Mkoani vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi 463,000/=.




Akikabidhi vifaa hivyo kwa rais wa klabu hiyo, Msaidizi Kiongozi wa timu ya Madaktari hao Wu Zheng Can,alisema serikali ya watu wa China na serikali ya Zanzibar zitaendeleza urafiki wao wa udugu wa muda mrefu.


Kiongozi huyo, alisema iko haja ya kuanzishwa timu za watoto wadogo kwa vile watarithi kutoka kwa wazee wao watakapoondoka na timu hiyo itadumu kwa muda mrefu.


Alisema timu nyingi duniani zinakuwa endelevu na zenye ushindani mkubwa kutokana na kuwepo kwa timu za watoto, ambao hupikwa na kuiva kimichezo.


Alifahamisha Serikali ya watu wa China , haitokuwa tayari kuiona Zanzibar , inakuwa nyuma katika sekta mbali mbali ikiwemo Michezo na Utamaduni jambo ambalo linawezekana kuendelezwa na kudumishwa.


Mapema kiongozi mkuu wa timu ya Madaktari wa Kichina walioko katika Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba, CHEN ER DONG, alieleza mbali na kutoa huduma za afya pia wanajumuika na wanajamii katika mambo mbali mbali yakiwemo elimu , michezo na utamaduni .


Aidha aliishukuru jamii ya watu wa Mkoani kwa ushirikiano wao unaopelekea kudumu kwa urafiki huo na kupatikana faida mbali mbali zinzochohea maendeleo ya nchi .
chanzo Zanzibar leo

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top