Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar imepokea ujumbe kutoka Kampuni ya Kimataifa ya China ijulikanayo
kama ‘China National Offshore Oil Corporation (CNOOC)’ inayojishughulisha na
uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia.
Viongozi wa Kampuni
hiyo wamefika katika Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Zanzibar huko Forodhani
Mjini Unguja na kufanya mazungumzo na wenyeji wao ikiwa ni miongoni mwa
utekelezaji wa makubaliano yao juu ya suala la mafuta na gesi asilia visiwani
humu .
Akizungumza kuhusu
ziara ya ujumbe huo wa (CNOOC) visiwani humu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Maji,
Nishati na Mazingira Zanzibar, Ali Khalili Mirza alisema ujumbe huo ni
utekelezaji wa makubaliano ambayo Kampuni hiyo ilitiliana saini na Serikali ya
Mapunduzi ya Zanzibar mwaka jana juu ya suala la mafuta na gesi asilia.
“Uongozi wa kampuni
hii ambayo ni kubwa katika anga za masuala ya mafuta duniani hasa katika
utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi imetuma viongozi wake hawa kwa lengo
kudumisha ushirikiano kati yao na Serikali yetu ya Mapinduzi Zanzibar”alisema .
Mizrai alisema kuwa
kazi kubwa ya kampuni hiyo visiwani hapa kwa hatua ya kwanza itaanza na utoaji
wa mafunzo kwa wafanyakazi mbali mbali wa masuala ya mafuta mafunzo ya muda
mfupi na mrefu wakiwa chini ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
“ Katika hati yetu ya
makubaliano tuliyoweka kati yetu na kampuni hiyo ni inaonesha kuwa pamoja na kazi nyengine lakini
pia viongozi hao watapata nafasi ya kutoa mafunzo ya kwa wataalamu wa Zanzibar
wataoshughulika na sekta ya Gesi na Mafuta”alisema Mizrai.
Aidha Wataalamu hao
kutoka Zanzibar pia watapata nafasi ya kwenda nchini China kupata mafunzo zaidi
kuhusiana na Mafuta na gesi asilia.
“ kampuni ya
(CNOOC) imeweza kuonana na Waziri na wamekuja hapa kuweza kusalimiana nae kama
nyumbani na baadae wataweza kuonana na viongozi mbali mbali wanaohusika na
sekta ya Mafuta na Gesi ”alisema Katibu Mkuu.
Kuhusu hatua ya
uchimbaji wa Mafuta iliyofikiwa hapa Zanzibar Katibu Mirza alisema bado suala
hilo lipo katika hatua ya utafiti na kwamba Wataalamu watakapomaliza taarifa ya
matokeo ya utafiti itatolewa kwa Wananchi.
Facebook Blogger Plugin by Piere
Post a Comment