KAMATI ya Maendeleo ya Wanawake, Habari na Utalii Baraza la Wawakilishi, imeelezea kusikitishwa kwake na ufinyu wa bajeti iliyotengwa katika sekta ya michezo nchini.



Mwenyekiti wa kamati hiyo Ali Suleiman Ali (Shihata) wakati akiwasilisha ripoti ya kamati hiyo katika kikao cha baraza la wawakilishi huko Chukwani.

Alisema serikali inafahamu kwamba timu zinashiriki mashindano ya kimataifa kila mwaka lakini fedha zinazotengwa ni kidogo na hazisaidia klabu zinazoshiriki.

Alisema kutokana na bajeti ndogo inayotengewa baraza la michezo, watendaji wa baraza hilo wanabakia kuwa omba omba kwa wafanyabiashara jambo ambalo haliweza kusaidia kukuza kiwango cha michezo nchini.



Hivyo ameomba kuongezwa bajeti katika sekta hiyo ili kusaidia klabu zinaposhiriki mashindano ya kimataifa

Aidha kamati hiyo imeendelea kutoa pongezi kwa timu ya soka ya taifa Zanzibar (Zanzibar Heroes), pamoja na timu ya soka ya ufukweni (Zanzibar Sand Heroes), kwa kufanya vyema katika mashindano ya Afrika Mashariki.

 

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top