TIMU ya Kipanga ilikubali kuachia pointi tatu kwa Kilimani City baada ya kupokea kipigo cha mabao 2-1, kwenye mchezo wa Ligi Kuu Zanzibar uliopigwa uwanja wa Amaan saa 10:00 jioni.

Pambano hilo zuri na la kupenda lilihudhuriwa na watazamaji wachache huku timu hizo zikicheza kandakanda safi kila mmoja akitafuta mabao ya ili kupata pointi tatu muhimu.

Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika tayari Kilimani City ilikuwa ikiongoza kwa mabao hayo mawaili yaliofungwa na Rajab Ali dakika ya 31 pamoja na Chande Abdalla dakika ya 41.

Kipindi cha pili Kipanga ilikuja juu na kuanza kupanga mashambulizi ili kusawazisha mabao hayo, lakini waliambulia kupata bao la kufutia machozi lililofungwa na Sabri Ali dakika ya 78.

Wakati huo huo Ligi Kuu kanda ya Pemba timu ya Chipukizi imeendelea kufufua matumaini yake ya kucheza hatua ya nane bora,baada ya kuitandika timu ya Kizimbani mabao 2-1.

Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Gombani, huku ukishuhudiwa na mashabiki wengi wa soka, Chipukizi imeweza kupanda hadi katika nafasi ya sita kutoka nafasi ya nane ikifikisha pointi 26.

Timu hizo ilikianza kipindi cha kwanza kwa kasi kubwa, kila timu ikilisakama lango la mwenzake , ambapo Kizimbani ilikuwa ya kwanza kuliona lango la wapinzani wao dakika ya 29 kupitia kwa Abdalla Hamad, na Chipukizi ikasawazisha bao hilo kupitia kwa Abdalla Mohamed dakika ya 39 na huku bao la pili likifungwa na Salum Abdalla.

Hata hivyo kuingia kwa goli hilo wachezaji wa timu ya Kizimbani walimjia juu mshika kibendera nambari moja Tahir Silima, kwa madai kuwa kabla ya bao kufungwa tayari alikuwa ameshanyanyua bendera juu.

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top