SERIKALI imefanikisha mradi wa upelekaji huduma za umeme katika visiwa vyote vya Zanzibar vinavyoishi watu na inatarajiwa ifikapo mwaka 2020 utafika  katika maeneo yote.

Hayo  yalielezwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Nishati, Ardhi na Mazingira, Ali Khalili Mirza, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  kufuatia kukamilika upelekaji umeme kisiwa cha Fundo, uliogharimu shilingi bilioni 2.1.

Alisema  upelekaji umeme katika  kisiwa hicho umekamilika na tayari  zaidi ya wanachi 300 wameshaungiwa huduma hiyo na uungaji wa umeme kwa wananchi waliobakia unaendelea.

Alisema umeme ni moja ya kichocheo kikubwa cha maendeleo ya wanachi,hivyo serikali inafanya jitihada kufanikisha huduma hiyo.

Aidha alisema kukamilika upelekaji umeme katika kisiwa hicho ni ahadi ya  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ya kukipatia umeme  kisiwa hicho katika sherehe za mapinduzi mwaka 2017.

Alisema uunganishaji huo ulianza kijiji cha  Ukunjwi  na umepita  chini ya bahari hadi  Fundo kwa kiasi cha kilomita 2.4 na waya uliozama kilomita 1.7.

Alisema lengo la serikali ni kuwapelekea wananchi wake  huduma zote muhimu katika  maeneo yao,hivyo aliwataka wananchi wa Fundo kuitumia vyema huduma hiyo.

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top