Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu
Antipas Lissu amewasili katika uwanja wa ndege jijini Brussels, nchini
Ubelgiji ambapo amepelekwa kwa ajili ya awamu ya tatu ya matibabu yake
yatakayohusisha mazoezi ya viungo.
Tundu Lissu amewasili jijini hapo
akitokea katika Hospitali ya Nairobi, nchini Kenya alikokuwa anapatiwa
matibabu kwa muda wa takribani miezi minne sasa, kutokana na
kushambuliwa kwa risasi.
Mbunge Tundu Lissu, ambaye pia ni
Mnadhimu Mkuu wa kambi ya Upinzani Bungeni, alishambuliwa kwa risasi na
watu wasiojulikana, alipokuwa akitokea Bungeni, majira ya saa 7 mchana,
karibu na nyumbani kwake Area D, Mjini Dodoma.
Kwa Mujibu wa taarifa ya madaktari
waliokuwa wanamtibu, walieleza kuwa jumla ya risasi 16 zilimpata Tundu
Lissu mwilini mwake, na wamefanikiwa kuzitoa, isipokuwa moja ambayo iko
nyuma ya uti wa mgongo wake.
Tundu Lissu alieleza kuwa wataalamu na
madaktari wake walishauri kuwa risasi hiyo ni hatari zaidi kama
ikitolewa kuliko ikibaki ndani ya mwili wake, kutokana na eneo
ilipokwama,chanzo malunde.
Facebook Blogger Plugin by Piere
Post a Comment