JAJI Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu, amesema wamejipanga kuhakikisha wanaondoa mrundikano wa kesi mahakamani huku akitoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa mahakama pindi wanapohitajika kutoa ushahidi.

Alisema hayo katika hafla ya ufunguzi wa maadhimisho ya utoaji elimu ya sheria na siku ya sheria nchini, jijini Dar es Salaam.

Alisema Februari 6 mwaka huu wanatarajia kufungua mahakama Mwanakwereke, uzinduzi ambao utafanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein.
Alisema mahakama hiyo itasaidia kupunguza mrundikano na kesi kusikilizwa kwa haraka.

Kuhusu kuchelewa kwa kesi, alisema ifikapo Februari 15 kila hakimu na jaji atalazimika kuhakikisha anamaliza kesi kwa wakati na kwa wale watakaoishindwa waondoke ili kutoa fursa kwa wanaoweza.
Hata hivyo, alisema hadi sasa wanaendelea vizuri kwa kuwa hata kesi za udhalilishaji na dawa za kulevya zinasikilizwa haraka.

Pia alisema Zanzibar haipo nyuma katika utumiaji wa teknolojia na mahakama imeanzisha kitengo cha teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) ambapo Jaji Mkuu atakuwa na uwezo wa kujua kesi alizopangiwa kila Jaji na Hakimu na hatua zilipofikia.

Alisema, licha ya mafanikio hayo wanakabiliwa na changamoto ya bajeti.

Mapema Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Hamis Juma, aliwataka wananchi kufuata taratibu na misingi ya kimahakama na kusisitiza kuwa haki inapatikana kwa njia ya suluhu nyumbani.

Alisema kuna uelewa mdogo kwa baadhi ya wananchi kwamba ukienda mahakamani kutafuta haki lazima ushinde jambo ambalo si sahihi.

Alisema wananchi ni wadau wakubwa wa sheria kwa sababu sheria zipo kwa ajili yao lakini wanapokwenda mahakamani kutaka haki sio lazima washinde.

“Haki sio ushindi bali ni kusikilizwa kwa kufuata misingi ya katiba na sheria na kukupa nafasi ya kusikilizwa na kutolewa uamuzi na endapo utakuwa hujaridhishwa na maamuzi utakata rufaa na hiyo ndio haki,”alisema.

Alisema kama dhana ya haki itaeleweka itasaidia kupunguza msongamano na malalamiko mahakamani,chanzo Zanzibar leo

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top