RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, amesema kuwa hana mpango wa kuongeza muda wa kukaa madarakani baada ya muhula wake utapokamilika.

 

Dk. Shein, aliyasema hayo jana wakati akizungumza na Waandishi wa Habari, katika kiwanja cha Ndege cha Zanzibar, mara baada ya kuwasili nchini akitoka katika ziara yake aliyoifanya katika nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu.

 

Dk. Shein, alisema yeye anaiheshimu Katiba ya Zanzibar, hatoweza kufanya jambo hilo na hakuna mtu ataweza kumlazimisha ama kumvuta ili abakie madarakani baada ya muda wake kumalizika.

 

“Hili sijalisema, sitolisema na hakuna wa kunivuta, siku yangu ikifika nitaondoka mwenyewe nitamshika mkono Mama Shein tuondoke nakwenda zangu Kibele kupumzika”,alisema Dk. Shein.

 

Alisema amekuwa akiyasikia maoni ya wajumbe wa baraza la Wawakilishi, lakini huo ni mtazamo wao na hawezi kuwaingilia kwa vile utaratibu wa sasa ni kuheshimu katiba iliopo.

 

Alisema atahakikisha anaondoka madarakani, kwa vile bado kuna watu wengi ambao wanaweza kuchaguliwa kushika nafasi hiyo wakati wake utapofika.

 

Akizungumzia juu ya hoja ya marufuku iliyotolewa na serikali ya muungano juu ya kuzuiya usajili wa meli zinazofanyakazi nje ya nchi, alisema serikali itakaa kuangalia mapungufu ya sheria yaliopo katika usajili huo ili mataifa ya nje yasiweze kupata nafasi ya kuichezea Zanzibar.

 

Alisema hiyo ni kutokana na hapo awali serikali ililazimika kuufuta mkataba na kampuni ya Feltex baada ya kubaini kuwapo kwa kasoro ya kusajili meli ambazo nchi zao zilikuwa na vikwazo vya kimaaifa.

 

Alisema kutokana na hilo, kampuni hiyo iliamua kuifungulia kesi Mahakamani, lakini bado serikali inaendelea kulifanyia kazi suala hilo, ili kuona eneo hilo halina matatizo hapo baadae.chanzo Zanzibar leo

 

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top