RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, leo Jumapili anatarajiwa kuendelea kufungua mradi wa uzinduzi wa ukuta wa Forodhani uliopo Wilaya ya Mjini Unguja, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Dk. Shein, atafanya uzinduzi wa mradi huo, ambao utafanyika saa 10:00 za jioni na kusimamiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango.

Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi, katika sherehe hizo, leo anatarajiwa kufungua Tamasha la nne la Biashara Zanzibar, yatayofanyika Maisara Wilaya ya Mjini Unguja
Ufunguzi huo utafanyika saa 4:00 za asubuhi, ambapo Katibu Mkuu Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko, itasimamia kazi hiyo.

Sherehe hizo, pia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Haji Omar Kheir, leo anatarajiwa kufungua rasmi kituo cha Mafunzo na Usindikaji Mazao, utaofanyika katika Wilaya ya Chakechake kisiwani Pemba, ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za sherehe za Mapinduzi.

Ufunguzi huo, utafanyika katika Wilaya hiyo, saa 4:00 za asubuhi, ambapo Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, maliasili, Mifugo na Uvuvi, anatarajiwa kusimamia shughuli hiyo.

Nae, Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko, Balozi Amina Salum Ali, anatarajiwa kuweka jiwe la msingi la Ukumbi wa Mahafali SUZA, huko Tunguu Wilaya ya Kati Unguja.

Sherehe hiyo, intarajiwa kufanyika saa 4:00 za asubuhi, ambapo Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali anatarajiwa kuisimamia shughuli hiyo.

Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum, Juma Ali Khatib, katika sherehe hizo leo anatarajiwa kufanya uzinduzi wa Mradi wa maji safi na salama wa mazingira kwa kipengele cha ujenzi wa vyoo katika skuli za Zanzibar.

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top