WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, George Mkuchika amesema kuwa, ofisi yake haiungi mkono
mfumo wa kazi kwa mikataba.
Waziri Mkuchika ameongeza kuwa, mfumo huo ni gharama
kubwa ukilinganisha na kuajiri mfanyakazi kwa ajira ya kudumu na kwamba
wizara yake inashughulikia suala hilo na kwamba hivi karibuni taasisi za
umma hazitaruhusiwa kuajiri wafanyakazi wapya kwa mfumo wa mikataba.
“Tunataka kila ofisi kuajiri kwa mujibu wa mahitaji,
hatutaruhusu mfumo huu wa mikataba kuendelea kwa sababu ni gharama kubwa
mno kwa serikali,” alisema.
Kuhusu wafanyakazi wanaokwenda likizo maalum, waziri
alisema yeyote atakayekwenda katika likizo ya namna hiyo atatakiwa
kuwasilisha nyaraka zake wizarani lini anarudi na wale watakaowasilisha
barua kuwa wamerudi wanatakiwa kusubiri jibu la serikali.
“Kama ulikuwa nje ya nchi au ofisi mfano miaka mitano,
ni dhahiri kuna mtu alijaza nafasi yako, hivyo unaporudi, unatakiwa
kuwasilisha barua na kuipa nafasi serikali kujibu,” alifafanua Waziri
Mkuchika.
Ameeleza kwamba, suala la likizo maalum sio jambo jipya
katika mfumo wa utumishi wa umma na umekuwa ukitumika katika nchi
nyingi duniani.
“Hatuna shida nayo, lakini tunataka wafuate taratibu sahihi wanaporudi.”
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuchika amesema kuwa,
Bodi ya Mishahara na Maslahi (HSRB) iko katika hatua za mwisho za
kurekebisha mfumo mzima wa mishahara, utakaondoa tofauti ya uwiano wa
mishahara katika taasisi za umma kwa wafanyakazi wenye ujuzi, sifa na
uzoefu, by malunde
Facebook Blogger Plugin by Piere
Post a Comment