JESHI la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, limesema kuna ongezeko la kesi 58 za dawa za kulevya kwa mwaka 2017, kutoka kesi 36 ya mwaka 2016, kutokana na kuimarika operesheni mbali mbali zilizofanywa ndani ya mkoa huo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Kamanda wa polisi mkoa huo, Sheikhan Mohamed Sheikhan, alisema  mwaka 2016 ziliripotiwa kesi 36 za madawa ya kulevya, ambapo kwa mwaka 2017 kulikuwa na  kesi 94.

Alisema  mwaka 2017 kulikuwa na ongezeko la kesi 58 za dawa za kulevya sawa na asilimia 61.7, kutokana na msako mkali kwa watumiaji wa dawa hizo.

“Makosa ya dawa za kulevya yameongezeka kutoka 36 mwaka 2016 hadi 94 mwaka 2017, hii ni kutokana na juhudi kubwa ya kufanya msako katika mkoa wetu,” alisema.

Alieleza  mwaka 2016  kesi za dawa za kulevya zilikuwa 29, ambapo 14 zilifikishwa mahakamani, 11 ziko kwenye upelelezi, kesi saba zilipata hatia na moja imefungwa, huku makosa ya bangi yakiwa 65.

Alisema  kati ya kesi 94 za dawa za kulevya zilizoripotiwa mwaka 2017, kesi 31 zilipelekwa mahakamani, 45 ziko kwenye upelelezi, 10zilifugwa polisi na nane zilipata hatia.

Alisema  kwa kushirikiana na vikosi vya ulinzi na usalama wataendeleza juhudi za kukabiliana na vitendo hivyo ili kuhakikisha vinakomeshwa.

Chanzo, Zanzibar leo

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top