MAKAMU Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi(UWT),Thuwayba
Kisasi, amewaomba viongozi wa zamani wa jumuiya hiyo kuendelea kutoa maoni na
ushauri utakosaidia kuimarisha taasisio hiyo kisiasa, kiutendaji na
kiuongozi.
Ombi hilo amelitoa leo kwa
wakati tofauti alipowatembelea viongozi wa zamani wa jumuiya hiyo kwa lengo la
kupata ushauri unaotokana na uzoefu wao wa kisiasa na kiutendaji wa viongozi hao wa zamani waliowahi kuiongoza
taasisi hiyo kwa awamu tofauti.
Viongozi waliotembelewa ni pamoja na Bi. Fatma Mbarouk, Bi. Fatuma Theresa, Bi. Asha Mwinyi, Bi. Salma Yusuph, Bi. Mwantantu
Yusuph Shaaly pamoja na Bi. Johari
Yusuph Khatib.
Akizungumza baada ya
kuwatembelea Makamu Mwenyekiti huyo alisema bado jumuiya hiyo inathamini juhudi
za viongozi na watendaji hao waliowahi
kuongoza taasisi hiyo kwa mafanikio makubwa.
Makamu huyo aliongeza kuwa licha ya kupata
michango yao ya maoni katika namna ya kuendesha jumuiya pia nifaraja
kuwatembelea kwa lengo la kuwajulia hali na kwamba nao wanahisi faraja.
Katika maelezo yake
Thuwayba aliongeza kuwa haitaishia hapo kuwatembelea viongozi hao wa jumuiya
hiyo ambapo UWT itaendelea kuwawekea kipaumbele bila kuchoka.
"Nimejifunza mengi
kutoka kwa viongozi wetu wastaafu na wametushauri kuwa tuendelee kushikamana, tupendane na kufanya kazi zetu
kwa bidii.,"alifafanua Makamu huyo.
Aliongeza kuwa viongozi
hao wameshauri jumuiya hiyo iwe na Umoja, nguvu na kutoyumba kwa namna moja ama
nyingine na kwamba kufanya hivyo UWT itakuwa imara.
Facebook Blogger Plugin by Piere
Post a Comment