MTU mmoja amefariki dunia baada ya chombo chake alichokua akisafiria kupinduka na kuzama baharini.

Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 1:00 asubuhi Bumbwini Kiongwe wilaya ya kaskazini ‘B’ Unguja.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja, Hasina Ramadhan Taufik, alisema hayo wakati akizungumza na gazeti hilo.

Alimtaja marehemu huyo kuwa ni Warda Juma Ussi (17) mkaazi wa Bumbwini.

Alisema marehemu alikutwa na mauti akiwa anavua kwa kutumia mtumbwi ambapo chombo chake kilizama na kusababisha kifo chake.

Alisema mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi katika hospitali kuu ya Mnazimmoja na kukabidhiwa jamaa zake kwa mazishi.

Alitumia fursa hiyo  kuiomba jamii kuchukua tahadhari ili kuepuka ajali zisizo za lazima,chanzo Zanzibar leo

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top