Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Afisa Uandikishaji Wilaya ya Kaskazini
“B” MAKAME PANDU KHAMIS alisema zoezi la Uandikishaji wa Wapiga Kura
Wapya na uhakiki wa taarifa za Wapiga Kura linaendelea vizuri katika
Vituo vyote vya Wilaya ya Kaskazini “A” na vituo vya Shehia za Jimbo la
Donge.
Akizungumza wakati akitembelea vituo
hivyo, Afisa huyo alisema zoezi hilo linaendelea vizuri kutokana na
maandalizi na juhudi zinzochukuliwa na Watendaji wa Tume pamoja na
Masheha wa Shehia kuhamasisha Wananchi wao kwenda katika vituo
kujiandikisha na kuhakiki taarifa zao.
Aliongeza kusema kuwa, mpaka sasa Vituo
vyote 33 vya Wilaya ya Kaskazini “A” pamoja na Vituo tisa vya Jimbo la
Donge kuna Idadi Kubwa ya Wananchi waliojitokeza kuandikishwa na
kuhakiki taarifa zao mbali na baadhi ya changamoto ndogo ndogo
zilizojitokeza vituoni ambazo zilirekebishwa kwa kupewa maelekezzo
wapiga kura kwenda katika vituo ambavyo zipo taarifa zao.
Aidha, Ndugu Makame alieleza kuwa amani
na utulivu umetawala katika Vituo hivyo ambapo aliwataka wananchi
hususan Vijana ambao wametimiza sifa za kuwemo kwenye daftari kwenda
kujiandikisha na kwa wale waliokuwemo katika Daftari kwenda kuhakiki
taarifa zao kwani bila kufanya hivyo hawatoweza kupiga kura kwa Uchaguzi
Mkuu wa mwaka 2020.
Nao baadhi ya Mawakala wa vyama vya
Siasa katika vituo mbali mbali vya Uandikishaji vya Wilaya hiyo walisema
uandikishaji na uhakiki wa taarifa za Wapiga kura ni jambo la kitaifa
hivyo, kuna kila sababu ya kila mwananchi kwenda kujianddikisha ikiwa ni
hatua moja wapo ya kukuza Demokrasia nchini.
Wananchi ambao walifika katika vituo
kuomba kuandikishwa pamoja na kuhakiki walisema utulivu katika maeneo
hayo umewavutia zaidi kwenda katika vituo hivyo ambapo wamewaomba
wananchi ambao hajaandikisha wafanye hima kutumia fursa hiyo kabla ya
muda uliopangwana Tume kumalizika.
Zoezi la uandikishaji wa Wapiga Kura
Wapya na uhakiki wa taarifa za Wapiga Kura waliokuwemo katika Daftari la
Kudumu la Wapiga Kura kwa Wilaya ya Kaskazi “A” na Jimbo la Donge
unatarajiwa kumalizika Siku ya Jumatano ya tarehe 19/2/2020
Facebook Blogger Plugin by Piere
Post a Comment