JESHI la Polisi mkoa wa kusini Pemba limesema, katika muendelezo wa sheria kuchukua mkondo wake, Mahkama ya mkoa wa Chakechake imemuhukumu ustadhi Khamis Radhaman Ali miaka 25 mkaazi wa Mvumoni, kwenda chuo cha mafunzo miaka mitano (5), pamoja na kulipa fidia ya shilingi milioni 1.5 kutokana na kosa la ubakaji na kumpa ujauzito mwanafunzi wake wa miakak 14.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kamanda wa Polisi mkoa wa kusini Pemba, Shehan Mohamed Shehan alisema, ustadhi huyo, alikutikana na tukio hilo Febuari 2017 .

Alisema tukio hilo la ubakaji lilifanyika maeneo ya Miembeni Chakechake ndani ya Madrasa ambamo mtoto huyo na wenzake alikuwa akiwasomeshwa na mwalimu wao huyo.

Katika hatua nyengine Kamanda Shehan alisema , jana jeshi la polisi lilifanikiwa kumkamata kijana Khamis Maharuki Khamis miaka 21 wa Machomane Chakechake akiwa na misokoto 19 ya inayodhaniwa kuwa ni bangi.

“Kulikua na doria maalum, hivyo askari walimtilia mashaka kijana huyu na walipompekuwa ndipo walipomkuta na misokoto hiyo,” alisema Kamanda.

Aidha Jeshi la polisi limemkamata Maryam Abdallah Kuya wa Mgagadu akiwa na na pombe ya kienyeji lita 12 zikiwa katika begi la nguo zake, akitokea Mgagadu kwenda Wete.

Kamanda alisema , watuhumiwa wote wapo wapo chini ya mikono ya polisi, wakiendelea kuhojiwa ili sheria ichukue mkondo wake .

Sambamba na hayo kamanda amewataka wananchi wajiepushe na matendo ya uvunjifu wa sheria, hasa udhalilishaji na matumimizi ya madawa ya kulevya kwani jeshi la polisi mkoa limejipanga vya kutoasha kukabiliana na wavunjifu wote wa sheria.

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top