Mashindano ya mbio za baiskeli North Zanzibar Sportive   yatafanyika Agosti 19, Visiwani Zanzibar katika mkoa wa kaskazini  na kumalizika Nungwi huku zaidi ya washiriki 200 watakimbia Kilometa 50 na 100 kwa wanaume na wanawake.


Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na matayarisho hayo  Mkurugenzi wa Mbio hizo Abrahman Hussein amesema lengo la kuanzisha mashindano ni kuibua vipaji vya wakimbiaji wa mbio za Baskeli pamoja na kuisaidia Jamii ambapo wamepanga kusaidia ujenzi wa Skuli ya Chekechea ya Nungwi.


Amesema mashindano hayo yatasaidia kuongeza idadi ya Watalii nchini na kuongeza pato la taifa na wananchi mmoja mmoja pamoja na ongeza la ajira kwa vijana, na mashindano hayo pia yanamalengo ya kuleta umashuhuri kwa Zanzibar.


“Nia na madhumuni yetu ni kuutangaza utalii na kuitangaza Zanzibar kwenye mashindano ya Baskeli na tunawashukuru sana wadhamini wetu bila wao tusenge fanya haya ya leo” Alisema Abrahman .


Kwa Upande wao   Wadhamini wa Mashindano hayo wamesema wameamua kusaidia Mashindano hayo kwa kumfata Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohammed Shein ambae analengo la kurejesha vugu vugu la Michezo Zanzibar.


Aidha wadhamini hao wamesema wao ni wadau wakubwa wa mazingira Zanzibar na mashindano hayo yanaweza kutangaza mazingira na fursa za kwa vijana wa Nungwi kujitangaza ki utalii ni sehemu ya ajira kubwa kwa Zanzibar.


 Msemaji wa chama cha Baskeli Zanzibar (CHABAZA) Saleh Kijiba amesema mashindano hayo yamejumuisha wachezaji wa Zanzibar nzima kwani wapo wengine watakaotoka Kisiwani Pemba kushiriki Mashindano hayo.


“wachezaji wetu watakuwa kwenye rika tofauti pia tutakuwa na watoto watakao shindana kwenye mchezo huu kunzia miaka 13 kushuka chini watafanya maajabu mwaka huu” Alisema Kijiba.


Aidha Kijiba ameweka wazi washiriki wa mashindano hayo watakuwa ni wachezaji wa timu za Taifa ya Zanzibar za Baskeli na wazee wakunzia umri wa miaka 60 kwenda juu..


Katika Mashindano hayo ambayo yataanzia Nungwi, watapita Kiwengwa, Pwani Mchangani mpaka Pongwe kisha kurejea tena Nungwi walipoanzia ambapo washiriki wote watapatiwa zawadi ya Medali , huku mshindi wa kwanza atapatiwa Shilingi Milioni 1, nafasi ya pili Laki 5 na watatu Laki 3 kwa Wanaume na Wanawake.


Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top