Rais wa Zanzibar,Dk Ali Mohamed Shein amewataka waislam nchini kuacha tabia ya kubaguana kwa rangi au ukabili kwani kufanya hivyo kuondosha Umoja uliopo miongoni mwa wanajamii.

Alisema si Jambo la busara miongoni mwa waislamu kutokea mtu kumbagua mwenzio kwa rangi yake au kabila lake .

Dk Shein alitoa nafasa hizo leo huko Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja wakati akizungumza na waislam katika baraza la Eid .

Alisema ili nchi kufikia malendeleo ya kweli hakuna budi kwa waislam kuwa wamoja katika kila Jambo la kuleta maendeleo.

Hivyo alisema haungi mkono hata kidogo kuona Kuna watu wanabaguana hasa katika masuala ya uislam.

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top