Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameinasihi Jamii Nchini kuwa na tahadhari kubwa wakati wa matumizi ya vifaa vya umeme ili kuwepuka madhara yanayoweza kuleta maafa makubwa hapo baadae.


Alisema Huduma ya umeme ni nzuri na muhimu katika matumizi ya mwanadamu kwenyea harakati zake na kimaisha za kila siku lakini inaweza kuwa janga iwapo mwanaadamu huyo ataamua kutumia huduma hivyo ovyo.


Balozi Seif Ali Iddi alitoa nasaha hizo muda mfupi tu alipopata taarifa ya kutokea kwa Janga la Moto katika Nyumba ya Familia ya  Marehemu Maalim Rajab Mgeni iliyopo Rahaleo mbele ya Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Muembe Shauri.


Hata hivyo hakuna mtu aliyepata matatizo kutokana na mripuko wa moto huo uliosababishwa na kuungua kwa Hita iliyokuwemo kwenye Nyumba hiyo ambayo wakati inawaka alikuwemo Kijana Mmoja wa familia ya Marehemu Maalim Rajab Mgeni.


Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuzingatia umuhimu wa kulinda maisha na mali za Rais imeazimia kujenga Vituo vya Huduma za Zimamoto kila Wilaya kwa lengo la kuwa tayari wakati yanapojitokeza matukio ya majanga.


Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top