Baraza la Mtihani Tanzania (NECTA) leo limetangaza matokeo ya kidato cha sita ambapo katika matokeo hayo Necta imezuia matokeo ya watahiniwa kumi na tatu kutokana na sababu kadhaa na wengine nane kufutiwa kabisa matokeo kwa sababu ya udanganyifu.

Akitaja sababu za kuzuiwa kwa matokeo hayo, Katibu mtendaji wa baraza hilo Dkt. Charles Msonde wakati akitangaza matokeo hayo leo visiwani Zanzibar, amesema kuwa kuna baadhi ya watahiniwa walishindwa kukamilisha mitihani yao kutokana na sababu za kiafya na hivyo kufanya mitihani nusu, watapewa nafasi ya kurudia mwaka unaofuata.

Bonyeza hapa kuangalia matokeo ya kidato cha 6- 2018

Licha ya hiyo, Dkt. Msonde amesema kuwa ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 96.06% mwaka 2017 hadi 97.12% mwaka huu, huku ufaulu katika masomo ya sayansi umeshuka ukilinganishwa na masomo ya sanaa na biashara.

Jumla ya watahiniwa 83,581 sawa na asilimia 97.58 ya watahiniwa waliofanya mitihani ya kidato cha sita Mei mwaka huu wamefaulu huku wasichana wakiwa ni 34,358, na wavulana waliofaulu ni 49,223 pekee”, amesema Dkt. Msonde.

Dkt. Msonde ameongeza kuwa tathmini ya hali ya matokeo imeonesha kuimarika kwa ufaulu katika madaraja ya I,II na III ikiwemo kupanda kwa asilimia 1.80 kutoka 93.72 mwaka 2017 na kuwa asilimia 95.52 mwaka 2018.

Shule zilizofanya vizuri zimetajwa kuwa ni Kibaha, Kisimiri, Kemebos na Mzumbe, Feza Boys, Marian Boys, AHMES, St Mary’s Mazinde Juu, Marian Girls & Feza Girls.

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top