WAKAAZI wa manispaa wilaya magharibi ‘B’ wametakiwa kuwa waangalifu wanaponunua vyakula hususan vya maji vinavyouzwa katika viwanja vya sikukuu ili kujikinga na maradhi ya mripuko ikiwemo kipindupindu.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kwamchina, Mkurugenzi wa baraza hilo, Amour Ali Mussa, alisema wamefanya ukaguzi viwanja vyote 10 vinavyotarajiwa kufanyika sikukuu ili kuhakikisha wafanyabiashara wanazingatia masharti ya afya.

Alisema hali ya maandalizi ya viwanja hivyo yako vizuri lakini bado wananchi wanahitajika kuchukua tahadhari wanaponunua vyakula.

Alieleza kuwa wamejaribu kuweka watu wa afya kila kiwanja kwa lengo la kuangalia usalama wa afya kutokana na kuwa hawajaaminisha usafi wa vyakula kwa baadhi ya maeneo ya kufanyia biashara hizo.

Alisema baraza limeweka polisi jamii katika viwanja ili kusaidia pale matatizo yanapojitokeza na kuwaomba wananchi kutoa taarifa watakapobaini wauza vyakula wanakiuka masharti ya afya.

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top