NEPAL: Watu kadhaa wanahofiwa kufariki baada ya ndege ya Bangladesh airline(Bombardier Q400) iliyokuwa na abiria 67 pamoja na wafanyakazi 4 kuwaka moto ilipokuwa inatua uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Tribhuvan, Jumatatu ya leo.
Taarifa zinasema watu 17 wameokolewa na wamepelekwa hospitali kwa matibabu huku miili mingi ikiwa imelazwa chini.
Ndege hiyo iliyokuwa inatokea Dhaka ilishika moto mara moja baada ya kugusa ardhi wakati inatua kwenye njia yake, hivyo kupoteza uwelekeo na kuanguka.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya hali ya hewa nchini Nepal, Sanjiv Gautam amesema kuwa ndege haikuwa na udhibiti wakati ilipojaribu kutua. Alisema ndege iliruhusiwa kutua kutokea upande wa Kusini lakini imetoka upande wa Kaskazini.
chanzo,jamiiforums
Facebook Blogger Plugin by Piere
Post a Comment