Watu 16 wamepoteza maisha nchini Rwanda baada ya kupigwa na radi wakiwa kanisani katika wilaya ya Nyaruguru iliyo Kusini mwa nchi hiyo.

Watu wote 140 waliokuwa katika kanisa hilo walipelekwa hospitali, lakini wengi waliruhusiwa kurudi nyumbani, isipokuwa watatu ambao bado wako katika hali mahututi.

Meya wa wilaya ya Nyaruguru Habitegeko Francois, amesema kuwa siku moja kabla, Radi nyingine ilikuwa imepiga kundi la wanafunzi 18 katika wilaya hiyo, na kuuwa mmoja wao.

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top