WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Amali, imemsimamisha kazi mwalimu wa skuli ya msingi ya Sebleni, Zuwena Mwinyi Haji, kwa kosa la kukiuka maadili ya ualimu.

Inadaiwa mwalimu huyo amejipiga picha na kujirusha kwenye mtandao wa kijamii katika mazingira yenye kuondosha heshima.

Naibu Katibu Mkuu wizara hiyo (taaluma) Madina Mjaka Mwinyi, alieleza hayo wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake Mazizini.

Alisema kwa hatua za awali wizara imemsimamisha kazi na kumtaka ajieleze ndani ya wiki moja ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.

Aidha alisema, kitendo alichofanya ni kinyume na kanuni 32(c),(d) ya sheria ya utumishi wa umma ya mwaka 2014 na kanuni ya 3 na 4 (kanuni za miiko ya maadili ya kazi za ualimu mwaka 1996).

Alisema, suala alilolifanya mwalimu huyo haliwezi kuvumilika wala kufumbiwa macho hasa ikizingatiwa limekiuka utaratibu wa maadili ya ualimu pamoja na silka na mila za Wazanzibari.

chanzo, zanzibarleo

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top