WATU wawili wakaazi wa Mkoa wa Tanga wanashikiliwa na jeshi la polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba baada ya kukamatwa wakiwa na mafurushi 25  ya majani makavu yanayosadikiwa kuwa ni bangi yenye uzito wa kilo tano na nusu.

Watuhumiwa hao ni Seif Yussuf Msumari na Shadia Stephano wakaazi wa Tanga.

Akizungumza ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Haji Khamis Haji, alisema watuhumiwa hao wamekamatwa na askari katika eneo la bandari ya Wete.

Alisema jeshi la polisi bado linaendelea kuwahoji watuhumiwa na upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinawakabili.

“Kwa sasa tunaendelea kuwahoji na upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma ambazo zinawakabili,”alisema.

Alsiema kwa upande wa jeshi la polisi wamejipanga kuendesha misako na operesheni sehemu za bandari, madago na maeneo mengine yanayodhaniwa kutumika kupitisha dawa za kulevya.

“Hizi operesheni tunazoendelea nazo ni endelevu, lengo ni kuhakikisha wananchi wanaishi salama bila ya kutumia dawa za kulevya,”alieleza.

Aidha aliwaomba wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa sahihi ambazo zitafanikisha kuwakamata wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
Chanzo Zanzibar leo

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top