Mama mmoja mwenye umri wa miaka73 amefafiki dunia baada ya kunasa katika waya wa umeme huko Tumbatu Mtakuja Wilaya ya Kaskazini A.

 

Taarifa zilizopatikana kutoka kwa watu wakaribu na eneo la tukio ikithibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja Hasina Ramadhan Tawfik amemtaja marehemu huyo kuwa ni Tatu Makame Hajji  ambapo majira ya saa nne dakika thelathini asubuhi marehemu kabla hajapatwa na ajali hiyo alikua akienda kazini ambapo alikuwa njiani kuelekea huko ndipo aliponasa katika waya wa umeme ambayo nguzo yake imekatika.

 

Kufuatia kutokea kwa tukio hilo Kamanda Hasina Ametowa wito kwa jamii kuwa makini wakati wanapokuwa katika shuhuli zao ili kujiepusha na majanga kama hayo.Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi Hospitali na kukabidhiwa jamaa zake kwa mazishi.

chanzo, Znz 24

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top