RAIA wa Argentina, Eduardo Mariselo Baiban (48) amekutwa amekufa katika hoteli ya Tembo iliyopo Shangani mjini  Unguja.

Akito taarifa kwa vyombo vya habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Hassan Nassir Ali, alisema raia huyo alikutwa amefariki ndani ya chumba chake alichokuwa amepangisha.

Alisema wafanyakazi ndani ya hoteli hiyo wakati wanakwenda kufanya usafi, walimkuta marehemu huyo akiwa amefariki na kutoa taarifa kwa uongozi wa hoteli hiyo.

Alisema mwili wa marehemu ulifikishwa katika hospitali kuu ya Mnazimmoja kwa ajili ya uchunguzi.

Alisema maiti hiyo imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hadi pale jamaa zake watakapofika ili kufanyiwa uchunguzi kujua chanzo cha kifo chake.

Kwa upande wa makosa ya usalama barabarani, alisema makoa 456 yalikamatwa ambapo 191 yalipelekwa mahakamani na kuingiza shilingi 8.3.

Aidha alisema wiki iliyopita ajali tatu ziliripotiwa na kusababisha majeruhi na uharibifu wa mali  na kati ya ajali hizo moja ilisababisha kifo.
chanzo, zanzibar leo

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top