Jeshi la Polisi limefanikiwa kumtia mbaroni, Hassan Abultalib maarufu ‘kiringo’ baada ya kutuhumiwa kumlawiti mtoto wa kiume miaka ‘13’.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Unguja , Hassan nassri Ali alisema kuwa Kiringo anatuhumiwa kufanya tukio hilo huko Fuoni Mjini Unguja baada ya kudaiwa kumnyesha kilevi kijana huyo hatimae kumfanyia kitendo kiovu cha kumlawiti.

Kamanda Nassir alisema kuwa Polisi wamefanikiwa kumtia mikononi mtuhumiwa huyo akiwa katika harakati za kutaka kusafiri uwanja wa ndege Mjini Unguja kwenda Mwanza Tanzania bara.

Alisema kuwa kazi kubwa iliyofanikiwa kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo ni umoja wa vyombo vya ulinzi na usalama kufanya kazi zake kikamilifu akisema kuwa hakuna mtu mwenye uwezo wa kukivikimbia vyombo vya usalama.

Kwa mujibu kamanda huyo Kiringo yupo mikononi mwa Polisi katika kituo cha Polisi Fuoni kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria dhidi yake.

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top