ZURA inapenda kuwatoa khofu Wananchi kuwa hakuna Uhaba wa Mafuta, ifuatayo ni hali halisi ya Akiba ya Mafuta iliyopo Zanzibar kwa mujibu wa Taarifa za Tarehe 30/12/2017.
Akiba ya Mafuta kwa Jumla ni:-

*PETROLI:* Lita 624,802 sawa na mahitaji ya siku 4 hadi Tarehe 3 Januari 2018.

*DIESEL:* Lita 1,383,896 sawa na mahitaji ya kutosheleza siku 9 hadi Tarehe 8 Januari 2018.
*KEROSENE:* Lita 602,042 sawa na mahitaji ya siku 3 hadi Tarehe 02 Januari 2018.

Mahitaji ya Mafuta kwa siku: 
Petroli: Lita 165,000.
Diesel: Lita 152,000.
Kerosene: Lita 163,000.

Akiba ya Mafuta kwa Kampuni moja moja ni:

*ZANZIBAR PETROLEUM (ZP)*

Petrol: Lita 111,142 
Diesel: Lita 143,653
Kerosene: Lita 165,333

*UNITED PETROLEUM (UP)*

Petrol: Lita 513,660
Diesel: Lita 1,231,896
Kerosene: Lita 321,577

*GAPCO*

Petrol: Lita 109,498 (yamemaliza)
Diesel: Lita 469,898
Kerosene: Lita 115,132

Kampuni ya GAPCO ndiyo imepungukiwa na Mafuta ya Petroli, hata hivyo Juhudi zimeshachukuliwa na Meli inategemewa kupakia Mafuta Leo baada ya kucheleweshwa kupakia tokea juzi kutokana na kuwepo kwa foleni ya Meli inayopakia gesi hapo Dar es salaam kutokana na Skukuu za Krismas na Mwaka Mpya.
Tunaomba Wanachi wawe Watulivu kwasababu Mafuta yapo ya kutosha na hakuna haja ya kujaza Mafuta mengi kwenye Vyombo kwa kukhofia Uhaba wa Mafuta.

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top