RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amekutana na kufanya mazungumzo na Sheikh Mohammed bin Rashid Al Makhtoum, ambapo viongozi hao walijadili nyanja mbalimbali za ushirikiano baina ya nchi hizo.

Sheikh Mohammed ni makamu wa Rais na Waziri Mkuu wa nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu na mtawala wa Dubai, ambapo kiongozi huyo aliahidi na Zanzibar katika sekta mbalimbali za maendeleo ikiwemo biashara, uwekezaji na utalii.

Katika maelezo yao viongozi hao walieleza azma ya kuendeleza uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu ambao ni wa kihistoria uliopo kati ya Zanzibar na Dubai.

Kwa upande wake, Dk. Shein alimueleza kiongozi huyo juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Zanzibar katika kuhakikisha sekta ya utalii inaimarika sambamba na ongezeko la watalii wanaovitembelea visiwa vya zanzibar.

Dk. Shein alisema ongezeko la wataalii kwa sasa wanavitembelea visiwa vya Zanzibar linaweza kuvuka watalii 500,000 kabla ya kufikia mwaka 2020.

Alimueleza kiongozi huyo huyo vivutio kadhaa vya asili vilivyopo Zanzibar vikiwemo Mjimkongwe uliobeba na kusheheni historia kubwa, fukwe za bahari, bidhaa viungo, utamaduni, mazingira na ukarimu wa Wazanzibari.

Alieleza mikakati mbalimbali inayotekelezwa katika kuhakikisha sekta hiyo inaimarika zaidi ili kunufaisha wananchi na kukuza uchumi wa Zanzibar.

Aidha Dk. Shein alimueleza kiongozi huyo hatua zinazoendelea kuchukuliwa katika kuimarisha sekta ya uwekezaji na biashara hasa ikizingatiwa kuwa Zanzibar ina historia kubwa ya kibiashara kati yake na nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu.

Alitumia fursa hiyo kueleza umuhimu wa shirika la ndege la Emirate kufanya safari kati ya Dubai na Zanzibar ili kuzidi kuimarisha sekta hizo.

Nae Sheikh Mohammed bin Rashid Al Makhtoum alimuhakikishia Dk. Shein kuwa atahakikisha juhudi za zinachukuliwa katika kuhakikisha uhusiano kati ya pande mbili hizo unaimarishwa.

Alimueleza Dk. Shein kuwa nchi yake inathamini ushirikiano uliopo na kuahidi kuuendeleza kwa kuunga mkono juhudi za serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha sekta za maendeleo ikiwemo utalii, uwekezaji na biashara.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya ndege ya Emirate, Sheikh Ahmed Bin Saeed Al Makhtoum alimuhakikishia Rais Dk. Shein kuwa kampuni ya ndege ya Fly Dubai itaongeza safari zake kati ya Zanzibar na Dubai.

Wakati huo huo, Dk. Shein alifanya mazungumzo na jumuiya ya wafanyabiashara, wawekezaji na wenye viwanda wa Dubai na kuwakaribisha nchi kuwekeza miradi yao.

Dk. Shein aliwataka wawekezaji hao wa Jumuiya ya Wafanyabiashara, wawekezaji na wenye viwanda wa Dubai kuchangamkia fursa za uwekezaji zilizopo Zanzibar.

Aliwahakikishia kuwa Tanzania na Zanzibar kwa jumla kuna usalama na amani ya kutosha jambo ambalo limekuwa ni chachu ya maendeleo yanayoendelea kupatikana hivi sasa.

NA RAJAB MKASABA, DUBAI

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top