MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA), ina mpango wa kujenga ofisi mpya za kisasa, ili kuimarisha utendaji wa kazi zao pamoja na kutoa huduma nzuri kwa wateja.
Ujenzi huo utakaohusisha majengo mawili pacha, unatarajiwa kufanywa katika maeneo ya Maisara mjini Unguja katika kiwanja nambari saba na nane, ambapo harakati za kupatiwa Mkandarasi kwa ajili ya ujenzi zinaendelea.
Kaimu Mkurugenzi huduma kwa wateja wa ZURA, Mussa Ramadhan Haji, aliyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake Maisara, katika jengo la mfuko wa barabara.
Alisema harakati zote za matayarisho ya ujenzi wa majengo hayo tayari zimefanyika ikiwemo uuzaji wa zabuni na kilichobakia ni mchakato wa kumpata mzabuni atakaejenga majengo hayo. Alisema jumla ya zabuni 15 zilinunuliwa, 14 kati hizo zilirejeshwa.
Alisema majengo hayo yatakuwa ya ghorofa saba kila mmoja na yanatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miaka mawili ambapo ujenzi unatarajiwa kuanza Febuari mwaka huu.
Alisema mara baada ya ujenzi huo kukamilika, moja kati ya majengo hayo litatumiwa na Wizara ya Maji, Ujenzi, Nishati na Mazingira na jengine litakuwa ni ofisi za ZURA.
Alisema, lengo la ZURA kujenga majengo hayo ni kuwa na sehemu nzuri ya kuwapa utulivu wa kiutendaji wafanyakazi wake pamoja na kutoa huduma katika mazingira mazuri.
Hata hivyo, alisema bado ni mapema kutaja gharama zitakazotumika katika ujenzi huo,
by zanzibar leo
Facebook Blogger Plugin by Piere
Post a Comment