TIMU ya Simba leo ina kazi kubwa na ngumu pale itakapojitupa katika uwanja wa Amaan, kucheza na URA ya Uganda kutafuta tiketi ya kuingia hatua ya nusu fainali ya mashindano ya kombe la mapinduzi saa 10:00 jioni.

Katika mchezo huo ambao ni wa kumalizia hatua ya makundi, Simba italazimika kushinda kwa zaidi ya mabao mawili ili iweze kufuzo hatua ya nusu fainali.

Hadi sasa Simba ina pointi nne na URA ina pointi saba hatua ambayo itaifanya Simba, hata ikishinda watalazimika kupenya nafasi ya nusu kwa kuangaliwa mabao ya kufunga na kufungwa.

Mazingira hayo magumu kwa Simba yalikuja baada ya juzi usiku kukubali kipigo cha bao 1-0, kutoka kwa mabingwa watetezi wa kombe hilo.

Katika mchezo huo sifa zimuendee mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji chipukizi Iddi Kipwagile aliyefunga dakika ya 59 akimalizia pasi ya kiungo Frank Domayo ‘Chumvi’.

Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi tisa ikikamilisha mechi zake nne za Kundi A kwa ushindi wa mechi tatu na kufungwa moja na URA ya Uganda.

Simba inabaki na pointi zake nne baada ya mechi tatu, ikishinda moja na sare moja.

Kocha Mrundi wa Simba SC, Masudi Juma alitoa walinzi wengi na kuingiza washambuliaji wengi kipindi cha pili kulazimisha bao la kusawazisha, lakini Azam FC walikuwa makini kuzuia mashambulizi yote.

Na sifa zaidi zimuendee kipa Mghana, Razack Abalora aliyeokoa michomo mingi ya hatari hata akashinda tuzo ya Mchezaji Bora wa mechi baada ya mchezo huo.

Mchezo uliotangulia wa Kundi B, Singida United iliibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya JKU mabao ya Daniel Lyanga dakika ya 19 na Elinywesia Sumbi dakika ya 20.

Singida United wanafikisha pointi 12 baada ya mechi zao nne na watakamilisha mechi zao za Kundi B kwa kumenyana na Yanga SC inayoshika nafasi ya pili kwa pointi zake tisa Jumatatu. Singida na Yanga zimekwishafuzu Nusu Fainali,chanzo zanzibar leo

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top