BEIJING, CHINA
WATU 32 hawajulikani waliko baada ya meli ya mafuta na ile ya mizigo kugongana mashariki mwa pwani ya China.
Meli ya mafuta ya Sanchi yenye usajili wa Panama ikibeba tani 136,000 za mafuta kutoka Iran ilishika moto baada ya kugongana.
Wizara ya uchukuzi nchini China ilisema kuwa watu ambao hawakulinai wali ni wahudumu wa meli wakiwemo 30 raia wa Iran na wawili kutoka Bangladesh.
Hata hivyo wahudumu 21 wa meli ya mizigo walifanikiwa kuokolewa.
Meli nane za China zilitumiwa katika oparesheni ya uokoaji kwa mujibu wa shirika la habari Xinhua la China.
Aidha Korea Kusi
ni nayo imetuma meli ya walinzi wa pwani na helikopta kusaidia katika uokoaji.
Meli ya mizigo ya usajili wa Hog Kong CF Crystal ilikuwa imebeba tani 64,000 za nafaka kutoka Marekani kwenda mkoa wa Guangdong kusini mwa China. BBC
Facebook Blogger Plugin by Piere
Post a Comment