WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Khalid Salum Mohammed, amesema  Zanzibar imepiga hatua kubwa  kwenye sekta ya afya ikilinganishwa na nchi za Afrika  huku ikiendelea  na jitihada za kuongeza madaktari bingwa pamoja na vituo vya afya mijini na vijijini.

Alieleza hayo alipokua akizungumza na gazeti hili kuhusu mafanikio ya serikali katika huduma za kijamii kwa mwaka 2017 ofisini kwake Vuga.

Alisema serikali itahakikisha huduma ya afya zinaimarika na dawa muhimu zinapatikana kwa wingi katika maeneo yote ya kutolea huduma.

Alisema zoezi la usomeshaji madaktari linaendelea ambapo wapo waliopelekwa nchini Cuba na wengine nchi nyengine zenye uwezo mkubwa wa ufundishaji katika fani hiyo.

Aidha alisema huduma za maji safi na salama zimeimarika licha ya kuwepo changamoto katika baadhi ya maeneo.

Kwa mfano, alisema katika jimbo la Donge anakotokea  upatikanaji wa  huduma za afya na maji unaimarika ambapo kwa hatua ya awali,  wataimarisha nyumba za madaktari pamoja na kuhakikisha vifaa muhimu vya afya vinapatikana kulingana na mahitaji ya wananchi.

Alisema, mapema mwaka 2018 atafanya zoezi maalumu la kuwafikishia elimu ya afya wananchi wa jimbo hilo ili watambue umuhimu wa utunzaji wa afya  na kuepuka kutumia vyakula vinavyoweza kuhatarisha afya zao.

Pia alisema amejipanga kununua gari ya wagonjwa ili kuondosha changamoto ya usafiri wakati wagonjwa wanapohitaji kupelekwa hospitali ya Mnaziimmoja au Kivunge.

Kuhusu kilimo, alisema serikali imetenga bajeti ya ununuzi wa mbolea kwa ajili ya kilimo cha mpunga ambapo wakati wowote itawasili.

Alisema pia serikali itahakikisha inaongeza matrekta mengine mapya ili kuondosha changamoto zinazojitokeza wakati msimu wa kulima.

Aliwataka wakulima kutumia fursa ya ruzuku ya mbolea ya asilimia 75 inayotolewa na serikali kwa ajili ya uimarishaji wa kilimo cha kisasa.

Aliwahimiza wafanyakazi  wanaosimamia fedha kuon

Chanzo, Zanzibar leo

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top