MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imetoa vitambulisho 500 kwa wananchi kutoka shehia mbali mbali za Unguja tokea kuanza tamasha la nne la biashara lililoanza Januari 10 katika viwanja vya Maisara mjini Unguja.

Ofisa  Habari Mwandamizi wa NIDA, Said Mohammed Said, aidha alisema watu 70 wamesajiliwa tokea kuanza tamasha hilo.

Alisema shehia ambazo wananchi waliopatiwa vitambulisho hivyo wanatoka ni  Mkunazini, Kiponda, Shangani, Kikwajuni Juu, Kikwajuni Bondeni, Kisimamajongoo, Kisiwandui, Malindi, Shangani Mwembetanga, Vikokotoni, Miembeni, Kilimani, Urusi  na Jang’ombe.

Alisema shughuli ya usajili wananchi zinaendelea katika maonesho hayo pamoja na kutoa elimu kuhusu umuhimu wa vitambulisho kwa wananchi.

Alisema maonesho ya mwaka huu ni mazuri lakini chanagamoto kubwa iliyopo ni wananchi kwenda kwa   makundi kujiandikisha hasa nyakati za asubuhi na jioni.

Aliwaomba wananchi waliosajiliwa Zanzibar kwenda katika ofisi za wilaya kwa ajili ya kufuatilia na kuchukua vitambulisho vyao.

Aliwahimiza kuvitunza na yeyote atakaekipoteza italazimika kuchangia shilingi 20,000 kwa ajili ya kutengezewa chengine.
Chanzo, Zanzibar leo

Facebook Blogger Plugin by Piere

Post a Comment

 
Top